• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 18, 2021

  AL AHLY WAICHAPA KAIZER 3-0 NA KUTWAA UBINGWA WA 10 AFRIKA

  TIMU ya Al Ahly ya Misri imefanikiwa kutwaa tena taji la Ligi ya Mbingwa Afrika baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini usiku huu Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
  Iliwabidi Ahly kusubiri hadi beki wa Kaizer Chiefs, Happy Mashiane atolewe kwa kadi nyekundu dakika ya 45 ili kuanza kushangilia mabao yao yaliyowapa taji la 10 la michuano hiyo.
  Kiungo Mohamed Sherif aliifungia Ahly bao la kwanza dakika ya 53 akimalizia pasi ya Akram Tawfik kabla ya yeye mwenyewe kuwasetia Mohamed Magdi Kafsha kufunga la pili dakika ya 64 na Amr Al Sulaya la tatu dakika ya 74.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AL AHLY WAICHAPA KAIZER 3-0 NA KUTWAA UBINGWA WA 10 AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top