• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 28, 2021

  NI RAJA NA JS KABYLIE FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

  TIMU ya Raja Athletic imeingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa Pyramids FC ya Misri kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya jumla ya 0-0.
  Baada ya sare nyingine ya 0-0 usiku wa jana Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca kufuatia sare ya wiki iliyopita ya 0-0 pia Jijiji Cairo, Raja wakakata tiketi yao ya fainali kwa matuta na sasa watakutana na JS Kabylie ya Algeria Julai 10A nchini Benin.
  Kabylie yenyewe imeitoa Cotonsport de Garoua ya Cameroon kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya ushindi wa 3-0 usiku wa jana Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers kufuatia ushindi wa 2-1 wiki iliyopita ugenini.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI RAJA NA JS KABYLIE FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top