• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 27, 2021

  NI AL AHLY NA KAIZER CHIEFS FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  MABINGWA watetezi, Al Ahly wamefanikiwa kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Esperance ya Tunisia usiku huu Uwanja wa WE Al-Ahly Jijini Cairo nchini Misri.
  Mabao ya Ahly yamefungwa na Ali Maâloul kwa penalti dakika ya 38, Mohamed Sherif dakika ya 56 na Hussein El Shahat dakika ya 60 na kwa matokeo hayo wanaenda fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza Jumamosi iliyopita Tunisia. 
  Al Ahly sasa itakutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo imeitoa Wydad Athletic baada ya sare ya 0-0 leo Johannesburg kufuatia ushindi wa 1-0 Jumamosi iliyopita Morocco.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI AL AHLY NA KAIZER CHIEFS FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top