• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 08, 2021

  CAF YASOGEZA MBELE MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KWA AFRIKA

  KAMATI ya Dharula ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa ushauri wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeamua kusogeza mbele mechi za kufuzu Kombe la Dunia barani kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).
  Taarifa ya CAF imesema kwamba mechi hizo zilizopangwa kuchezwa Juni mwaka huu sasa zitachezwa kuanzia Septemba, Oktoba na Novemba mwaka huu hadi Machi mwakani.
  Tanzania imepangwa Kundi J kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar mwakani kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 18 pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Benin na Madagascar.


  Na kwa mujibu wa ratiba mpya itaanza na Madagascar kati ya Septemba 5 na 8, kabla ya kucheza na DRC kati ya Septemba 1 hadi 4, Benin Oktoba 6 na 9 na marudiano Oktoba 10 na 12.
  Baada ya hapo itamenuana na DRC kati ya Novemba 11 na 13 na kukamilisha mechi zake za mchujo wa kundi hilo kwa kumenyana na  Madagascar kati ya Novemba 14 an 16.
  Baada ya hapo washindi wa makundi 10 watamenyana baina yao nyumbani na ugenini kupata wawakilishi watano wa Afrika kwenye fainali hizo za Qatar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAF YASOGEZA MBELE MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top