• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 29, 2021

  AL AHLY YATWAA SUPER CUP BAADA YA KUICHAPA BERKANE 2-0 QATAR

   TIMU ya Al Ahly ya Misri imefanikiwa kutwaa taji la Super Cup ya Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya RSB Berkane  Uwanja wa Jassim Bin Hamad, au Al-Sadd Jijini Doha nchini Qatar.
  Mabao ya Ahly yamefungwa na Mohamed Sherif dakika ya 57 akimalizia pasi ya Hussein El Shahat na Salah Mohsen dakika ya 82 akimalizia pasi ya Taher Mohamed.
  Mechi ya Super Cup hukutanisha bingwa wa Ligi ya Mabingwa ambaye kwa sasa ni Al Ahly na bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, ambaye ni Berkane.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AL AHLY YATWAA SUPER CUP BAADA YA KUICHAPA BERKANE 2-0 QATAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top