• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 22, 2021

  AHLY WAITOA MAMELODI NA KUTINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

   MABINGWA watetezi, Al Ahly ya Misri wametinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya  1-1 na wenyeji, Mamelodi Sundowns jioni ya leo Uwanja wa Lucas Masterpieces Moripe Jijini Pretoria, Afrika Kusini. 
  Ahly walitangulia kwa bao la Yasser Ibrahim dakika ya 11, kabla ya Mosa Lebusa kuisawazishia Mamelodi dakika ya 30 na kwa matokeo hayo mabingwa hao watetezi wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya kushinda 2-1 kwenye mechi ya kwanza wiki iliyopita Cairo.
  Timu nyingine iliyotinga Nusu Fainali hadi sasa ni Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini iliyoitoa Simba SC ya Tanzania kwa jumla ya mabao 4-3.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AHLY WAITOA MAMELODI NA KUTINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top