• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 14, 2021

  ONYANGO ASTAAFU KUICHEZEA THE CRANES BAADA YA MIAKA 15

  NYOTA wa Uganda na Nahodha, kipa Denis Onyango ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa, The Cranes baada ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka 15.
  Onyango, kipa namba moja wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini anakuwa mchezaji wa pili kujiuzulu The Cranes mwezi huu baada ya kiungo wa ulinzi, Hassan Wasswa Mawanda anayechezea Jeddah SC ya Saudi Arabian aliyetangaza uamuzi wake wiki iliyopita
  Na Onyango anastaafu baada ya kuiedakia The Cranes katika mechi 79 tangu alipoanza kuichezea timu hiyo mwaka 2005 katika mechi dhidi ya Cape Verde.
  Kisoka aliibukia Nsambya FC, kabla ya kwenda SC Villa zote za kwao, Uganda baadaye St George ya Ethiopia, Supersport, Black Aces, Bidvest Wits na Mamelodi Sundowns za Afrika Kusini.


  Onyango atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa ulioiwezesha Uganda kucheza Fainali mbili za Kombe la Mataifa ya Afrika, Gabon mwaka 2017 na Misri 2019.
  Baada ya kuiwezesha Mamelodi Sundowns kutwaa taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa wa Afrika mwaka 2016 – alishinda ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika mwaka huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ONYANGO ASTAAFU KUICHEZEA THE CRANES BAADA YA MIAKA 15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top