• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 13, 2021

  DK PATRICE MOTSEPE WA AFRIKA KUSINI NDIYE RAIS MPYA WA CAF

  RAIA wa Afrika Kusini, Dk. Patrice Motsepe amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika Mkutano Mkuu wa 43 wa CAF uliofanyika jana Jijini Rabat, Morocco.
  Dk Motsepe, ambaye anakuwa Rais wa saba wa CAF, ambaye ataliongoza shirikisho hilo kwa miaka minne ijayo baada ya kupita bila kupingwa kufuatia kujitoa kwa Augustin Senghor, Ahmed Yahya na Jacques Anouma.
  Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Mtaliano Gianni Infantino aliyehudhuria uchaguzi huo Jijini Rabat alizitaka nchini wanachama wa CA kuendeleza umoja waliouonyesa wiki chache zilizopita.


  Dk. Motsepe, mwenye umri wa miaka 59, ni mfanyabiashara mkubwa Afrika Kusini, ambayepia ni mfadhili na si mgeni mwenye soka. 
  Kwa miongo takriban miwili, amekuwa Rais wa klabu uya Mamelodi Sundowns ya kwao, Afrika Kusini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DK PATRICE MOTSEPE WA AFRIKA KUSINI NDIYE RAIS MPYA WA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top