• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 01, 2021

  NI MOROCCO NA CAMEROON NUSU FAINALI CHAN JUMATANO

  MABINGWA watetezi, Morocco na Guinea wote wamekwenda Nusu Fainali za michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2021 baada ya kuzitoa Zambia na Rwanda jana nchini Cameroon.
  Morocco iliitoa Zambia kwa kuitandika mabao 3-1 Uwanja wa Reunification Jijini Douala, mabao yake yakifungwa na Soufiane Rahimi dakika ya kwanza, Mohammed Ali Bemammer dakika ya nane na Ayoub El Kaabi kwa penalti dakika ya 39.
  Bao pekee la Zambia inayofundishwa na kocha Mserbia, Milutin Sredojevic 'Micho' lilifungwa na Moses Phiri dakika ya 80.


  Na bao pekee la Morlaye Sylla dakika ya 60 likaipa Guinea ushindi wa 1-0 dhidi ya Rwanda katika mchezo mwingine wa Robo Fainali Uwanja wa Limbe.
  Nusu Fainali zitachezwa Jumatano; Mali na Guinea Saa 12:00 jioni Uwanja wa Omnisport Jijini Douala na Morocco na Cameroon Uwanja wa Limbe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI MOROCCO NA CAMEROON NUSU FAINALI CHAN JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top