• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 08, 2021

  MOROCCO MABINGWA TENA CHAN, WAICHAPA MALI 2-0 CAMEROON

  MOROCCO wamefanikiwa kutwaa tena taji la michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mali jana Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde, Cameroon.
  Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo, beki wa  Hassania Agadir, Soufiane Bouftini dakika ya 69 akimalizia pasi ya beki wa RSB Berkane, Omar Nemssaoui na mshambuliaji wa Wydad Casablanca, Ayoub El Kaabi dakika ya 79 akimalizia pasi ya kiungo wa Ittihad Tanger, Mohammed Ali Bemammer. 
  CHAN inaendelea kuweka maskani Kaskazini mwa Afrika, ambako limedumu tangu 2011 lilipochukuliwa na Tunisia, baadaye Libya 2014 na Morocco 2018, wakati bingwa mwingine wa CHAN ni DRC mara mbili 2009 na 2016.
  Guinea juzi walifanikiwa kumaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Cameroon mabao ya kiungo Morlaye Sylla dakika ya tisa na mshambuliaji Mamadouba Bangoura dakika ya 45 na ushei Uwanja wa Reunification Jijini Douala.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOROCCO MABINGWA TENA CHAN, WAICHAPA MALI 2-0 CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top