• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 07, 2021

  GUINEA YAICHAPA CAMEROON 2-0 NA KUMALIZA YA TATU CHAN

  TIMU ya Guinea jana walifanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Cameroon Uwanja wa Reunification Jijini Douala.
  Fainali ya CHAN, michuano inayoshirikisha wachezaji wanaocheza nchini mwao pekee inafanyika leo kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde, ikiwakutanisha mabingwa watetezi, Morocco na Mali #ZBC2.
  Kwa miaka mitatu mfululizo taji hilo limeweka maskani Kaskazini mwa Afrika, Tunisia (2011) Libya (2014) na Morocco (2018) zikipokezana.


  Bingwa mwingine wa CHAN ni DRC mara mbili 2009 na 2016 – wakati mafanikio makubwa ya Mali ni kufika fainali 2016 nchini Rwanda ambako walichapwa 3-0 na DRC.
  Mabao ya Guine jana yalifungwa na kiungo Morlaye Sylla dakika ya tisa na mshambuliaji Mamadouba Bangoura dakika ya 45 na ushei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GUINEA YAICHAPA CAMEROON 2-0 NA KUMALIZA YA TATU CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top