• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 09, 2021

  BEKI WA RWANDA AONDOKA ARMENIA, ATUA UJERUMANI

  BEKI Mnyarwanda ameachana na timu yake Armenia kwenda Ujerumani Nirisarike Salomon, beki wa kati wa Rwanda aliyeichezea FC Pyunik huko Armenia, tayari ameachana naye baada ya mwaka mmoja na nusu.
  Septemba 1, 2019, mchezaji aliyeichezea AFC Tubuze nchini Ubelgiji alisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya daraja la kwanza FC Pyunik huko Armenia.
  Baada ya kucheza kwa miezi 3, Desemba 2019 timu hiyo ilimuongezea mkataba wa mwaka mmoja.
  Beki huyo, ambaye amekuwa akiichezea klabu hiyo kwa mwaka mmoja na nusu, amebakiza mkataba wa miezi sita lakina wameamua kuachana kwa ajili ya timu hii ina shida kifedha.
  Kupitia mitandao yake, FC Pyunik imethibitisha kuachana na  Nirisarike na kumtakia mafanikio mema.


  Akizungumza na Bin Zubeiry, Nirisarike Salomon alijizuia kutangaza nchi na timu atajiunga nayo ambapo alisema atatangaza baada ya kupimwa afya.
  "Nategemea kupimwa afya baadaye nikasaini, vyote vikiwa tayali nitawaambia timu na nchi." Nirisarike
  Hadi sasa, ripoti zinaonyesha kuwa mchezaji huyo anaweza kwenda Ujerumani katika daraja la pili.
  Kuhamia kwake nchini ingekuwa sio mara ya kwanza kutakiwa na timu ya huko kwa sababu kabla ya kuhamia FC Pyunik mwanzoni mwa 2019 alikuwa akitafutwa na Fortuna Dusseldorf ambaye inacheza kwa daraja la pili nchini Ujerumani.
  Salomon, ambaye alikulia katika chuo cha mpira wa miguu cha Isonga, alihamia Royal Antwerp nchini Ubelgiji 2012, 2014 alikwenda Sint-Truidense, 2016 hadi 2019 alikuwa mchezaji wa AFC Tubize, 2019 akaenda FC Pyunik.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI WA RWANDA AONDOKA ARMENIA, ATUA UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top