• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 17, 2021

  AL AHLY YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA, YAICHAPA MERREIKH 3-0


  MABINGWA watetezi, Al-Ahly jana imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Al-Merreikh ya Sudan Uwanja katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
  Mabao ya mabingwa hao mara tisa Afrika yalifungwa na kiungo Mohamed Magdi Kafsha dakika ya 57 na washambuliaji, Mmisri mwenzake Mahmoud Abdul Monem Abdelhamid Soliman ‘Kahraba’ dakika ya 63 na Mzambia, Walter Bwalya dakika ya 71.
  Sasa washindi hao watatu wa Klabu Bingwa ya Dunia na watasafiri kuja Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wao wa pili wa kundi hilo dhidi ya Simba SC Jumanne ijayo kabla ya kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kwa kucheza na AS Vita ya DRC Machi 5 Cairo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AL AHLY YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA, YAICHAPA MERREIKH 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top