• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 18, 2021

  USHINDI AIPA USHINDI DRC DHIDI YA MAJIRANI, KONGO CHAN

  BAO pekee la Chico Ushindi Wa kubanza jana lilitosha kuipa mwanzo mzuri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kuwachapa majirani, Kongo-Brazzaville 1-0 katika mchezo wa Kundi B Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) Uwanja wa Omnisport Jijini Douala, Cameroon.
  Mshambuliaji huyo wa TP Mazembe ya Lubumbashi, alifunga bao hilo dakika ya 47 akimalizia pasi ya mshambuliaji wa AS ya Kinshasa, Makabi Lilepo na sasa DRC wanaongoza Kundi kufuatia Libya kulazimishwa sare ya 0-0 na Niger katika mchezo mwingine wa kundi hilo jana.
  Michuano inaendelea leo kwa mechi nyingine mbili za Kundi C, Morocco na Togo Saa 1:00 usiku na Rwanda Saa 4:00 usiku Uwanja wa Reunification mjini Douala, Cameroon.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: USHINDI AIPA USHINDI DRC DHIDI YA MAJIRANI, KONGO CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top