• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 23, 2021

  UGANDA YAJIWEKA PAGUMU CHAN BAADA YA KUPIGWA NA TOGO

  UGANDA imejiweka kwenye nafasi ngumu ya kusonga mbele Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee baada ya kuchapwa 2-1 na Togo jana Uwanja wa Reunification Jijini Douala.
  Mabao ya Togo jana yalifungwa na SemiouLast Tchatakora dakika ya 48 akimalizia pasi ya Yendoutie Richard Nane aliyefunga bao la pili dakika ya 57 kwa usaidizi wa Ashraf Agoro, wakati bao pekee la Uganda lilifungwa na Saidi Kyeyune dakika ya 51 akimalizia kazi nzuri ya Shafiq Kagimu.
  Mechi nyingine ya Kundi C jana, Morocco ililazimishwa sare ya 0-0 na Rwanda hapo hapo Uwanja wa Reunification Jijini Douala.


  Sasa Morocco ndio inaongoza kundi hilo kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na Togo pointi tatu, Rwanda pointi mbili na Uganda pointi moja kuelekea mechi za mwisho wiki ijayo.
  Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi mbili, Zambia na Guinea Saa 1:00 usiku na Namibia na Tanzania Saa 4:00 Uwanja wa Limbe Jijini Limbe. Mechi za kwanza, Zambaia iliifunga Tanzania 2-0 na Guinea iliichapa Namibia 3-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UGANDA YAJIWEKA PAGUMU CHAN BAADA YA KUPIGWA NA TOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top