• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 27, 2021

  RWANDA YATINGA ROBO FAINALI CHAN, UGANDA YAKIONA CHA MOTO

  TIMU ya taifa ya Rwanda imefanikiwa kwenda Robo Fainali za michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Togo Uwanja wa Limbe nchini Cameroon jana.
  Mabao ya Rwanda jana yalifungwa na Olivier Niyonzima dakika ya 45, Jacques Tuyisenge dakika ya 60 na Ernest Sugira dakika ya 66, wakati ya Togo yalifungwa na Yendoutie Richard Nane dakika ya 38 na BilaliAkoro dakika ya 58.
  Kwa matokeo hayo, Rwanda inamaliza na pointi tano katika nafasi ya pili Kundi C, nyuma ya mabingwa watetezi, Morocco ambao jana waliichapa Uganda 5-2 na kumaliza na pointi saba.
  Togo imemaliza na pinti tatu, wakati Uganda imemaliza na pointi moja baada ya sare moja na Rwanda kwenye mechi ya kwanza na kufungwa mechi zilizofuata. 


  Mechi za Kundi D zinakamilisha Hatua ya awali ya CHAN 2021 leo, Tanzania na Guinea Uwanja wa Reunification Jijini Douala na Zambia na Namibia Uwanja wa Limbe kuanzia Saa 4:00 usiku.
  Tanzania yenye pointi tatu, inahitaji ushindi tu leo ili kwenda Robo Fainali, wakati Guinea yenye pointi nne sawa na Zambia kwao sare itatosha kuwavusha, wakati Namibia imekwishaaga mashindano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RWANDA YATINGA ROBO FAINALI CHAN, UGANDA YAKIONA CHA MOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top