• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 19, 2021

  MOROCCO YAANZA VYEMA CHAN, YAICHAPA TOGO 1-0

  MOROCCO imeanza vyema Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Togo 1-0 kwenye mchezo wa Kundi C Uwanja wa Reunification Jijini Douala.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee , Yahya Jabrane kwa penalti dakika ya 27 Uwanja wa Reunification Jijini Douala na sasa Morocco wanaongoza kundi hilo baada ya jana Rwanda kulazimishwa sare ya 0-0 na Uganda.
  Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi nyingine mbili za Kundi D, Tanzania na wa Zambia Saa 1:00 usiku na na  Guinea na Namibia kuanzia Saa  3:00 usiku.


  Baada ya leo, Taifa Stars itarudi uwanjani Januari 23 kumenyana na Namibia kabla ya na kukamilisha mechi zake za Kundi D kwa kucheza na Guinea Uwanja wa Reunification, Douala Januari 27.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOROCCO YAANZA VYEMA CHAN, YAICHAPA TOGO 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top