• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 22, 2021

  MECHI ZOTE ZA KUNDI B CHAN ZAMALIZIKA KWA SARE YA 1-1 CAMEROON

  MECHI zote za Kundi B Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zilizofanyika jana Uwanja wa Japoma Jijini Douala zilimalizika kwa sare ya 1-1.
  Muetaz Husayn alianza kuifungia Libya dakika ya sita akimalizia pasi ya Rabia Al Shadi, kabla ya Amede Masasi kuisawazishia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 90 na ushei akimalizia pasi ya William Likuta Luezi
  Naye Mapata Mouandza akaanza kuifungia Kongo dakika ya 35 akimalizia basi ya Hardy Alain Samarange Binguila kabla ya Mossi Issa Moussa kuisawazishia Niger dakika ya 70. 


  DRC inaendelea kuongoza Kundi B kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na Niger pointi mbili sawa na Libya, wakati Kongo inashika mkia ikiwa na pointi moja.
  Hatua ya makundi ya CHAN 2021 inaendelea leo kwa mechi nyingine mbili za Kundi C; Morocco na Rwanda Saa 1:00 usiku – na Uganda na Togo Saa 4:00 usiku Uwanja wa Reunification Jijini Douala.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI ZOTE ZA KUNDI B CHAN ZAMALIZIKA KWA SARE YA 1-1 CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top