• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 01, 2021

  MECHI YA MAHASIMU WA MALAWI YAAHIRISHWA KWA SABABU YA CORONA

  MECHI ya 67 ya mahasimu wa Blantyre msimu wa 2020/21 wa Ligi Kuu ya TNM Malawi imeahirishwa kutokana na athari za virusi vya corona katika kambi ya Nyasa Big Bullets FC.
  Mabingwa watetezi, Bullets walitarajiwa kumenyana na na mahasimu wao, Be Forward Wanderers Januari 2 Uwanja wa Kamuzu Stadium, Jijini Blantyre.
  Hata hivyo, Bodi ya Ligi Kuu nchini Malawi (SULOM) imetangaza kuahirisha mechi hiyo kutokana na wachezaji 10 wa Nyasa Big Bullets na kiongozi wao mmoja kupimwa na kukutwa na virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.


  Tangu Jumanne Bullets wamesimamisha mazoezi yao kuzuia uwezekano wa kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo.
  Bullets inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi nane baada ya kucheza mechi tano, ikiwa inazidiwa pointi tano na vinara, Mafco FC ambao wamecheza mechin saba.
  Timu hiyo inatarajiwa kuanza tena mazoezi Jumatatu ya Januari 4 baada ya kufanya vipimo vingine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI YA MAHASIMU WA MALAWI YAAHIRISHWA KWA SABABU YA CORONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top