• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 25, 2021

  MALI NA TOGO ZATANGULIA ROBO FAINALI CHAN 2021

  WENYEJI, Cameroon na Mali wametinga Robo Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kumaliza juu ya Burkina Faso na Zimbabwe katika Kundi A.
  Mali imeongoza kundi hilo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Zimbabwe jana, bao pekee la Demba Diallo dakika ya 11 Uwanja wa Japoma Jijini Douala hivyo kumaliza na pointi saba.
  Cameroon imemaliza nafasi ya pili baada ya sare ya 0-0 na Burkina Faso jana Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde na kumaliza na pointi tatu katika nafasi ya pili. 


  Burkina Faso imemaliza na pointi nne nafasi ya tatu na Zimbabwe imeshika mkia baada ya kufungwa mechi zote.
  Leo ni mechi za mwishi za Kundi B Kongo inamenyana na Libya Uwanja wa Japoma Jijini Douala na Niger na DRC Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde.
  DRC inaongoza Kundi B kwa pointi zakr nne ikifuatiwa na Libya pointi mbili sawa na Niger, wakati Kongo ina pointi moja.
  Kesho ni mechi za mwisho za Kundi C Uganda na Morocco Uwanja wa Réunification Jijini Douala na Togo na Rwanda Saa 4:00 usiku Uwanja wa Limbe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALI NA TOGO ZATANGULIA ROBO FAINALI CHAN 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top