• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 21, 2021

  MALI NA CAMEROON ZATOKA SARE, BURKINA FASO YAITOA ZIMBABWE

  WENYEJI, Cameroon watahitaji kushinda mechi ngumu ya mwisho dhidi ya Burkina Faso ili kwenda Robo Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Mali jana.
  Mshambuliaji wa Cotonsport, Salomon Charles Banga alianza kuifungia Cameroon dakika ya sita Uwanja wa Omnisport Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde, lakini beki wa Stade Malien Bamako, Issaka Samake akaisawazishia Mali dakika ya 12.
  Nayo Burkina Faso ikapata ushindi wa kwanza, ikiichapa Zimbabwe 3-1 hapo hapo Uwanja wa Omnisport Ahmadou Ahidjo.


  Mabao ya Burkina Faso yalifungwa na beki Issouf Sosso dakika ya 14, kiungo Claver Tiendrebeogo dakika ya 53 na beki Issiaka Ouedraogo dakika ya 67, wakati la Zimbabwe lilifungwa na beki Partson Jaure dakika ya 23. 
  Cameroon inaendelea kuongoza Kundi A kwa pointi zake nne sawa na Mali, ikifuatiwa na Burkina Faso yenye pointi tatu,wakati Zimbabwe inakuwa timu ya kwanza kuaga mashindano baada ya kufungwa mechi zote mbili za kwanza.
  Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi mbili za Kundi B, Libya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Saa 1:00 usiku na Kongo na Niger Saa 4:00 usiku Uwanja wa Omnisport Jijini Douala.
  Mechi za kwanza DRC iliichapa Kongo 1-0 na Libya ilitoka sare ya 0-0 na Niger.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALI NA CAMEROON ZATOKA SARE, BURKINA FASO YAITOA ZIMBABWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top