• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 26, 2021

  KONGO ZOTE ZATINGA ROBO FAINALI YA CHAN 2021

  MAJIRANI, Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wote wamekwenda Robo Fainali ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya mechi za mwisho za Kundi B jana nchini Cameroon.
  Bao pekee la Gautrand Ngouenimba dakika ya 50 liliipa Kongo ushindi wa 1-0 dhidi ya Libya Uwanja wa Japoma Jijini Douala na kumaliza na pointi nne nyuma ya DRC iliyoongoza kwa pointi zake saba.
  DRC yenyewe ilimaliza kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Niger Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde. Mabao ya Cameroon yalifungwa Johns Kadima Kabangu dakika ya 27 na Amede Masasi dakika ya 90 na ushei, wakati la Niger lilifungwa na Mossi Issa Moussa dakika ya 73.


  Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi za Kundi C; Uganda na Morocco Uwanja wa Reunification Jijini Douala na Togo na Rwanda Saa 4:00 usiku Uwanja wa Limbe. 
  Morocco inaongoza kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na Togo pointi tatu, Rwanda pointi mbili na Uganda pointi moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KONGO ZOTE ZATINGA ROBO FAINALI YA CHAN 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top