• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 20, 2021

  GUINEA YAANZA VYEMA CHAN, YAITANDIKA NAMIBIA 3-0

  GUINEA wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda hatua ya mtoano ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Namibia jana katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Omnisport mjini Limbe.
  Mabao ya Guinea jana yalifungwa na nyota wa Horoya, mshambuliaji Yakhouba Gnagna Barry mawili dakika ya 13 na 86  na kiungo Morlaye Sylla dakika ya 45 na kwa ushindi huo wanaongoza kundi kwa wastani wa mabao dhidi ya Zambia.
  Mechi nyingine ya kundi hilo kana, Zambia iliichapa Tanzania 2-0, mabao ya washambuliaji wa NAPSA Stars, Collins Sikombe kwa penalti dakika ya 64 na Emmanuel Chabula wa Nkwazi FC dakika ya 81.


  Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi mbili za Kundi A, Cameroon na Mali Saa 1:00 usiku na Burkina Faso na Zimbabwe Saa 4;00 usiku Uwanja wa Omnisport Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GUINEA YAANZA VYEMA CHAN, YAITANDIKA NAMIBIA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top