• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 30, 2021

  CAS YAMREJESHA AHMAD MADARAKANI KWA MUDA KAMA RAIS WA CAF

  MAHAKAMA ya usuluhishi wa michezo, CAS, imemrudisha kwa muda madarakani Ahmad Ahmad kama Rais wa Shirikisho la soka la Afrika, CAF.
  Novemba 19 mwaka jana, kamati ya maadili ya Shirikisho la soka duniani, FIFA, ilimfungia Ahmad kujihusisha na soka kwa miaka 5, baada ya kumkuta na hatia ya kukiuka kanuni za maadili za uongozi wa soka.
  Kifungo hiki kilikuwa na maana kwamba Ahmad hawezi tena kutetea nafasi yake katika uchaguzi mkuu wa CAF utakaofanyika Machi 12.


  Lakini alikata rufaa CAS na kuomba adhabu yake iondolewe kwanza hadi rufaa yake itakaposikilizwa.
  Ahmad alitaka afunguliwe ili apate muda wa kuchukua fomu ya kugombea katika uchaguzi mkuu wa CAF.
  CAS imepanga kuisikiliza rufaa yake Machi 2 mwaka huu, lakini kwa maagizo kwamba adhabu yake iondolewe na arudi madarakani hadi hukumu ya rufaa itakapotoka.
  Hii sasa itampa fursa Ahmad kuchukua fomu yake na kugombea.
  Katika kipindi ambacho hakuwa madarakani, majukumu yake yalikaimiwa na makamu wake, Constant Omari, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rais wa chama cha soka nchini humo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAS YAMREJESHA AHMAD MADARAKANI KWA MUDA KAMA RAIS WA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top