• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 31, 2021

  CAMEROON NA MALI ZATINGA NUSU FAINALI CHAN, KONGO ZOTE NJE

  WENYEJI Cameroon wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana Uwanja wa Omnisport Jijini Douala.
  Mabao ya Cameroon jana yalifungwa na Yannick N'Djeng dakika ya 29 na Felix Oukine Tcheoude dakika ya 41, wakati la DRC lilifungwa na Makabi Lilepo dakika ya 2.
  Nayo Mali ilifanikiwa kwenda Nusu Fainali baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Kongo katika mchezo mwingine wa Robo Fainali jana Uwanja wa Omnisport Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde.
  Fainali za CHAN zinatarajiwa kuendelea leo Morocco ikimenyana na Zambia Saa 1:00 usiku na Guinea na Rwanda Saa 4:00.


  Mshindi kati ya Morocco na Zambia atakutana na Mali katika na mshindi kati ya Guinea na Rwanda atamenyana na Cameroon katika Nusu Fainali Jumatano, wakati Fainali itafuatia Jumapili baada ya mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Jumamosi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAMEROON NA MALI ZATINGA NUSU FAINALI CHAN, KONGO ZOTE NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top