• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 17, 2021

  CAMEROON NA MALI ZASHINDA 1-0 MECHI ZA UFUNGUZI CHAN 2021

  WENYEJI, Cameroon wameanza vyema Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Zimbabwe kwenye mchezo wa Kundi A Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde, Cameroon.
  Pongezi kwa wafungaji wa bao hilo pekee, beki wa Cotonsport de Garoua, Salomon Charles Banga dakika ya 72. 
  Nayo Mali imeichapa Burkina Faso 1-0, bao pekee la Siaka Bagayoko dakika ya 70 kwenye mchezo mwingine wa Kundi A. 
  Fainali za CHAN zinatarajiwa kuendelea leo kwa mechi mbili za Kundi B; Libya na Niger kuanzia Saa 11:00 jioni na DRC na Kongo kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Japoma Jijini Douala na zote zitakuwa LIVE ZBC 2 ndani ya kisimbusi cha Azam TV.


  KUNDI A: Cameroon, Mali, Burkina Faso, Zimbabwe | KUNDI B: Libya, DRC, Kongo, Niger | KUNDI C: Morocco, Rwanda, Uganda, Togo | KUNDI D: Tanzania, Zambia, Guinea, Namibia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAMEROON NA MALI ZASHINDA 1-0 MECHI ZA UFUNGUZI CHAN 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top