• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 13, 2020

  BEKI WA MAMELODI SUNDOWNS AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

  BEKI wa Mamelodi Sundowns na timu ya taifa ya Afrika Kusini, Motjeka Madisha amefariki dunia kwa ajali ya gari.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA) leo imesema kwamba Madisha amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 25 baada ya ajali ya gari mapema leo.
  Rais wa SAFA, Dk. Danny Jordaan na kocha wa Bafana Bafana, Molefi Ntseki wamepokea kwa masikitoko makubwa msiba huo.

  Madisha anakuwa beki wa pili wa Sundowns kufariki kwa ajali ya gari ndani ya mwezi mmoja, baada ya Anele Ngcongca kupoteza maisha katika ajali kamahiyo mashariki kwa Jiji la Durban Novemba 23.
  Madisha aliichezea Afrika Kusini mechi 13, akifunga bao moja na alikuwa beki wa kati chaguo la kwanza wa kikosi cha Sundowns kilichoshinda taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 2016 ambacho pia kilifika Nusu Fainali mara moja na Robo Fainali mara mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI WA MAMELODI SUNDOWNS AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top