• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 13, 2020

  UGANDA YAIPIGA SUDAN KUSINI 1-0, CAMEROON YAICHAPA MSUMBIJI 4-1

  TIMU ya taifa ya Uganda jana iliibuka na ushindi wa mwembamba nyumbani wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo wa Kundi B kufuzu Fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2021 nchini Cameroon.
  Kwa ushindi huo, The Cranes wanafikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu na kuendelea kuongoza kundi hilo.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa St. Mary's, Kitende bao pekee la Uganda lilifungwa na mtokea benchi, Halid Lwaliwa zikiwa zimebaki dakika tano akimalizia kwa kichwa mpira wa adhabu uliopgwa na Karim Watambala.


  Nayo Cameroon ikaibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Msumbiji mjini Douala kwenye mchezo wa Kundi F. Mabak ya Cameroon yalifungwa na Vincent Abubakar mawili, Frank Zambo-Anguissa na Clinton Njie.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UGANDA YAIPIGA SUDAN KUSINI 1-0, CAMEROON YAICHAPA MSUMBIJI 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top