• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 17, 2020

  PRINCE DUBE WA AZAM FC AWATUNGU ALGERIA LAKINI WAFUZU AFCON

  MABINGWA watetezi, Algeria wamefuzu fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) licha ya sare ya 2-2 na wenyeji, Zimbabwe kwenye mchezo wa Kundi H Jijini Harare jana.
  Andy Delort na Riyad Mahrez waliitanguliza Desert Foxes kwa mabao ya mapema, kabla ya Knowledge Musona na nyota wa Azam FC ya Tanzania, Prince Dube kuisawazishia Zimbabwe.
  Matokeo hayo yanaifanya Algeria ifikishe pointi 10, wakati Zimbabwe inabaki nafasi ya pili na pointi zake tano kuelekea mechi mbili za mwisho.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, Botswana iliichapa Zambia 1-0, matokeo ambayo yanazidi kulifanya Kundi H liwe gumu.


  Katika mchezo mwingine, bao pekee la Tito Okello kwa penalti dakika ya 36 dhidi ya nchi aliyozaliwa, Uganda liliipa Sudan Kusini ushindi wa 1-0 Uwanja wa Taifa wa Nyayo, Nairobi katika mchezo wa Kundi B.
  Pamoja na ushindi huo, Sudan Kusini inaendelea kushika mkia kwenye kundi hilo, wakati Uganda inaendelea kuongoza kwa poini zakr saba kuelekea mechi mbili za mwisho.
  Timu zote zilimaliza pungufu, Uganda wakimpoteza Khalid Aucho aliyetolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 31 wakati Sudan Kusini ilimpoteza mtokea benchi, Saad Musa aliyeonyeshea kadi ya pili ya njano dakika ya 80.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PRINCE DUBE WA AZAM FC AWATUNGU ALGERIA LAKINI WAFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top