• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 11, 2020

  NYOTA WA JUVENTUS NA MARSEILLE WAITWA TUNISIA KUIKABILI STARS

  KOCHA wa Tunisia, Mondher Kebaier ametaja kikosi cha wachezaji 26 kuelekea mchezo na Tanzania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon mwaka 2021.
  Kiungo wa Zamalek, Ferjani Sassi na beki wa kushoto wa Al Ahly, Ali Maaloul watakaokutana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwezi huu ni miongoni mwa waliojumuishwa kikosini. 
  Kebaier pia amewaita Youssef Msakni, Wahbi Khazri na Nabil Makni katika safu yake ya ushambuliaji.
  Beki wa AEK Athens, Nassim Hnid alirejeshwa kikosini kabla ya kupimwa na kukuta na virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19, hivyo kuenguliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Saddam Ben Aziza wa Etoile du Sahel.


  Beki wa Le Havre, Ayman Ben Mohamed ambaye ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa mara mbili na Esperance yumo kikosini pia.
  Tai wa Carthage watamenyana na Taifa Stars Ijumaa wiki hii Uwanja wa Hamadi Agrebi Olimpiki mjini Rades, kabla ya kurudiana nao Dar es Salaam siku nne baadaye.
  Tunisia inaongoza Kundi J kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Tanzania na Libya zenye pointi tatu kila moja, wakati Equatorial Guinea ambayo haina pointi inashika mkia.
  Kikodi kamili cha Tunisia ni, makipa: Farouk Ben Mustapha (Esperance), Moez Ben Chrifia (Esperance), Ayman Dahmen (CS Sfaxien) na Elyes Damerji (Stade Rennais, Ufaransa)
  Mabeki: Wajdi Kechrida (Etoile du Sahel), Mohamed Dräger (Olympiakos, Ugiriki) Yassine Meriah (Rizespor, Uturuki), Dylan Bronn (Metz, Ufaransa), Saddam Ben Aziza (Etoile du Sahel), Montassar Talbi (Rizespor, Uturuki), Oussema Haddadi (Kasımpaşa, Uturuki) na Ali Maaloul (Al Ahly, Misri)
  Viungo: Ferjani Sassi (Zamalek, Misri), Ellyes Skhiri (FC Cologne, Ujerumani), Anis Ben Slimane (Brondbiy IF, Denmark), Aymen Ben Mohamed (Le Havre, Ufaransa), Seifeddine Khaoui (Olympique de Marseille, Ufaransa), Naim Sliti (Al-Ittifaq, Saudi Arabia), Marc Lamti (Hannover, Ujerumani), Elyes Jlassi (US Monastir), Hamza Rafia (Juventus, Italia), Mohamed Amine Ben Amor (Etoile du Sahel), Saad Bguir (Abha, Saudi Arabia)
  Washambuliaji: Wahbi Khazri (Saint-Étienne, Ufaransa), Nabil Makni (Chievo Verona, Italia), Youssef Msakni (Al-Duhail, Qatar)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NYOTA WA JUVENTUS NA MARSEILLE WAITWA TUNISIA KUIKABILI STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top