• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 05, 2020

  NI ZAMALEK NA AL AHLY FAINALI LIGI YA MABINGWA NOVEMBA 27

  WENYEJI, Zamalek wamefanikiwa kwenda Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali usiku wa jana Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
  Mabao ya Zamalek jana yalifungwa na Ferjani Sassi dakika ya 61 na Mostafa Mohamed mawili dakika ya 85 na 88, kufuatia Mkongo Ben Malango Ngita kuwatanguliza wageni kwa bao zuri dakika ya 47. 
  Zamalek wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada kushinda 1-0 Oktoba 18 Casablanca kwenye ya kwanza.


  Sasa watakutana na mahasimu wao wa Jiji, Al Ahly waliotinga fainali baada ya kuitoa Wydad Casablanca kwa jumla ya mabao 5-1, 2-0 ugenini na 3-1 nyumbani. 
  Fainali itapigwa Uwanja wa Borg El Arab Jijini Alexandria nchini Misri Novemba 27.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI ZAMALEK NA AL AHLY FAINALI LIGI YA MABINGWA NOVEMBA 27 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top