• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 16, 2020

  EQUATORIAL GUINEA YAICHAPA TENA LIBYA, SENEGAL YAFUZU AFCON

  TIMU ya taifa ya Equatorial Guinea imefufua matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Libya kwenye mchezo wa Kundi J jana mjini Bata.
  Bao pekee la Nzalang Nacional lilifungwa na Ivan Edu Salvador dakika ya 27 na kwa ushindi huo, wanapanda nafasi ya pili wakifikisha pointi sita, wakizidiwa tatu na vinara, Tunisia, wakati Libya inabaki na pointi tatu sawa na Tanzania. 
  Bao pekee la nyota wa Liverpool, Sadio Mane dakika ya 82 liliipa Senegal ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Guinea-Bissau kwenye mchezo wa Kundi I jana na kuwa timu ya pili kufuzu AFCON ijayo baada ya wenyeji, Cameroon.
  Nayo Comoro imeichapa Kenya mabao 2-1 Jijini Moroni katika mchezo wa Kundi G, hivyo kufikisha pointi nane na kuendelea kuongoza kundi hilo katika mbio za Cameroon 2021.
  Mabao ya Comoro yalifungwa na El Fardou Ben na Faiz Mattoir, wakati bao pekee la Kenya lilifungwa na Cliff Nyakeya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EQUATORIAL GUINEA YAICHAPA TENA LIBYA, SENEGAL YAFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top