• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 12, 2020

  EQUATORIAL GUINEA YAICHAPA LIBYA 3-2 KUFUZU AFCON 2021

  MTOKEA benchi Salomon Obama Ondo jana ameifungia bao la ushindi Equatorial Guinea ikiibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Libya kwenye mchezo wa Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Uwanja wa WE Al-Ahly Jijini Cairo.
  Kwa matokeo hayo, Equatorial Guinea inafikisha pointi tatu sawa na Libya na Tanzania, ambayo kesho itamenyana na vinara wa kundi hilo, Tunisia.
  Mabao ya mengine ya Equatorial Guinea yalifungwa na Jose Antonio Miranda na Pedro Obiang, wakati ya Libya yalifungwa na Sanad Al Warfali kwa penalti na Mohamed Bettamer.
  Nayo Senegal ikaendeleza wimbi la ushindi Kundi I baada ya kuichapa 2-0 Guinea Bissau mabao ya Sadio Mane kwa penalti kipindi cha kwanza na Opa Nguette kipindi cha pili Uwanja wa Lat Dior mjin Thies.

  Nayo Kenya ikalazimishwa sare ya 1-1 na Comoro waliomaliza pungufu ya mchezaji mmoja katika mchezo wa Kundi G Uwanja wa Moi Sports Centre Kasarani Jijini Nairobi.
  Youssouf M’changama alianza kuwafungia Comoro kipindi cha kwanza kabla ya Masud Juma kuisawazishia Kenya kipindi cha pili. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EQUATORIAL GUINEA YAICHAPA LIBYA 3-2 KUFUZU AFCON 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top