• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 28, 2020

  AHLY YAIPIGA ZAMALEK 2-1 NA KUTWAA TAJI LA TISA LIGI YA MABINGWA

  TIMU ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa taji la tisa la rekodi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya mahasimu wao wa nyumbani, Zamalek Uwanja wa KImataifawa Cairo, Misri usiku wa jana.
  Shujaa wa Al Ahly jana alikuwa ni Mohamed Madgy Afsha aliyefunga bao zuri la ushindi zikiwa zimesalia dakika nne mchezo kumalizika.
  Fainali hiyo ya mahasimu wa Cairo, ambayo inakuwa ya kwanza kukutanisha timu za nchi moja kwenye historia ya michuano hiyo, ilikaribia kumalizika kwa sare kabla ya Magdy kuwakabidhi Mashetani Wekundu taji.


  Amr Al Sulaya alianza kuifungia Al Ahly dakika ya tano, kabla ya Mahmoud Abdel Razek Fadlallah 'Shikabala' kuisawazishia Zamalek dakika ya 31. 
  Kwa Kocha Pitso Mosimane aliyejiunga na Ahly kiasi cha miezi mitatu iliyopita, hilo linakuwa taji lake la pili la Ligi ya Mabingwa, akiifunga timu ile ile baada ya awali kutwaa Kombe hilo mwaka 2016 alipokuwa Mamelodi Sundowns ya kwao, Afrika Kusini.
  Ahly pia imeendeleza rekodi ya kutofungwa na timu za nyumbani kwao kwenye Ligi ya Mabingwa, ikishinda mechi ya sita jana kati ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AHLY YAIPIGA ZAMALEK 2-1 NA KUTWAA TAJI LA TISA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top