• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 11, 2020

  ALGERIA YAENDELEZA UBABE KWA NIGERIA, YAICHAPA 1-0 AUSRTIA

  HATIMAYE soka imerejea Afrika baada ya mapumziko ya tangu Machi kufuatia mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19 na mechi kadhaa za kirafiki zimechezwa wikiendi hii.
  Katika marudio ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ta Afrika (AFCON) 2019, mabingwa wa Afrika Algeria kwa mara nyingine wamempiga Tai Mkubwa wa Nigeria 1-0 nchini Austria bao pekee la Wapiganaji wa Jangwani lilifungwa na beki Ramy Bensebaini.
  Sasa Algeria inafikisha mechi 19 za kucheza bila kufungwa, kwani mara ya mwisho walifungwa Oktoba 2018 ugenini na Benin na wanatarajiwa kutanua rekodi yao watakapomenyana na Mexico Jumanne nchini Uholanzi.

  Beki Ramy Bensebaini amefunga bao pekee Algeria ikiichapa Nigeria 1-0  

  Jijini Antalya, Uturuki, Mali imeitandika Ghana 3-0, mabao ya Hamari Traore, El Bilal Toure na Amadou Haidara na sasa watajaribu kuendeleza wimbi la ushindi watakapomenyana na Iran Jumanne.
  Nao Senegal ambao kocha wao, Aliou Cisse alilaizmika kutumia kikosi kipya kabisa baada ya wachezaji wengi aliowaita kujitoa, walichapwa 3-1 na Morocco Jijini Rabat.
  Mshambuliaji wa Liverpool na Mwanasoka Bora wa Afrika 2019, Sadio Mane alikutwa na Covid-19, wakati kipa Edouard Mendy na beki Kalidou Koulibaly walikosekana kwa sababu ya kuwa majeruhi.
  Mabao ya wenyeji yalifungwa na Selim Amallah kipindi cha kwanza, Youssef en Nesyri na Youssef el Arabi kipindi cha pili, kabla ya Ismaila Sarr kuwafungia Simba wa Teranga bao la kufutia machozi dakika ya 88.
  Morocco sasa watamenyana na Jamhuri Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jijini El Jadida, wakati Senegal watajaribu kurejesha heshima mbele ya Mauritania, ambao waliifunga Nayo Tunisia ikaichapa Sudan 3-0 Jijini Rades, mabao ya Saif-Eddine Khaoui dakika ya 17, Ali Maaloul dakika ya 25 na Anis Ben Slimane dakika ya 35, wote wakimalizia kazi nzuri ya Nahodha Wahbi Khazri. 
  Tunisia sasa watahamishia nguvu zao kwenye mchezo dhidi ya Nigeria nchini Austria, wakati Sudan watamenyana na Togo.
  Mechi nyingine, Kenya ikaichapa 2-1 Zambia, waliokuwa wanacheza mechi yao ya pili ya kirafiki ndani ya siku mbili wakitoka kuifunga Malawi 1-0.
  Mabao ya Kenya yalifungwa Tandi Mwape aliyejifunga dakika ya 16 na Cliff Nyakeya dakika ya 36, wakati la Zambia lilifungwa na Emmanuel Chabula dakika ya 80.
  Zambia watamenyana na Afrika Kusini katika mchezo ujao, ambao walitoka sare ya 1-1 na Namibia kwenye mchezo wao wa kwanza kirafiki.
  Burkina Faso iliichapa DRC 3-0 wakati Gambia iliifunga Kongo 1-0, huku Cameroon ikilazimishwa sare ya bila mabao na Japan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ALGERIA YAENDELEZA UBABE KWA NIGERIA, YAICHAPA 1-0 AUSRTIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top