• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 20, 2020

  AZIZ APIGA MBILI, RSB BERKANE YATINGA TENA FAINALI SHIRIKISHO

  MABAO ya penalti ya Nahodha, Mohammed Aziz moja kila kipindi yameipa RS Berkane ushindi wa 2-1 dhidi ya Hassania Agadir, zote za Morocco katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika usiku wa jana Uwanja wa Prince Moulay Abdallah Jijini Rabat na kutinga fainali kwa mara ya pili mfululizo.
  Berkane ambayo ilifungwa na Zamalek kwa penalti kwenye fainali ya msimu uliopita, sasa itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili leo kati ya Pyramids ya Misri na Horoya ya Guinea Jumaopili.
  Aziz alifunga mabao yake dakika ya 20 na 61, wakati bao pekee la Hassania ambayo jana ilipoteza mechi ya kwanza kati ya 12 za Kombe la Shirikisho msimu huu, bao lake lilifungwa na Imad Kimaoui dakika ya 30.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZIZ APIGA MBILI, RSB BERKANE YATINGA TENA FAINALI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top