• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 13, 2020

  SALAH APIGA HAT TRICK LIVERPOOL YAICHAPA LEEDS UNITED 4-3 ANFIELD

  MABINGWA watetezi, Liverpool wameuanza vyema msimu baada ya ushindi wa 4-3 dhidi ya Leeds United waliorejea Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.
  Lakini haukuwa ushindi mwepesi kwa kocha Mjerumani Jurgen Klopp, kwani iliwalazimu The Kops kusubiri hadi dakika mbili za mwisho kujihakikishia kuondoka na pointi zote tatu za mchezo huo.
  Na shujaa wa Wekundu hao wa Anfeld alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah aliyefunga mabao matatu, mawili kwa penalti dakika ya nne na 88 na lingine dakika ya 33, wakati bao lingine la Liverpool lilifungwa na beki Mholanzi, Virgil Van Dijk.

  Mohamed Salah amefunga mabao matatu Liverpool ikishinda 4-3 dhidi ya Leeds United Uwanja wa Anfield 

  Mabao ya Leeds iliyorudi Ligi Kuu msimu huu yamefungwa na Jack Harrison dakika ya 11, Patrick Bamford dakika ya 30 na Mateusz Klich dakika ya 66.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SALAH APIGA HAT TRICK LIVERPOOL YAICHAPA LEEDS UNITED 4-3 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top