• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 03, 2020

  MAN UNITED YAMSAJILI DONNY VAN DE BEEK KWA PAUNI MILIONI 40

  HATIMAYE Manchester United imefanikiwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, Donny van de Beek.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Mashetani Wekundu kwa ada ua uhamisho ya Pauni Milioni 40 kutoka kwa vigogo wa Uholanzi,  Ajax.
  Van de Beek aliyesaini mkataba wa miaka mitano, wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi, inaaminika atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 107,000 kwa wiki nje posho.

  Manchester United imefanikiwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, Donny van de Beek 

  Anakuwa mchezaji mpya wa kwanza kusajiliwa na kocha Ole Gunnar Solskjaer kuelekea msimu ujao na anatarajiwa kuunda safu nzuri ya kiungo Old Trafford pamoja na Paul Pogba na Bruno Fernandes.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAMSAJILI DONNY VAN DE BEEK KWA PAUNI MILIONI 40 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top