• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 28, 2020

  KOCHA MRENO PACHECO AREJEA KUINOA TENA ZAMALEK YA MISRI

  KOCHA Mreno, Jaime Pacheco amewasili Jijini Cairo, Misri juzi kwa ajili ya kuanza kuifundisha klabu bingwa mara tano Afrika, Zamalek.
  Pacheco, ambaye awali aliiongoza Zamalek kati ya Oktoba na Desemba mwaka 2014, amechukua nafasi ya Mfaransa Patrice Carteron, ambaye alijiuzulu ghafla mwezi uliopita na kuhamia Al Taawun ya Saudi Arabia.
  “Nimerejea Misri kwa sababu naipenda Zamalek. Lengo langu ni kushinda taji la Ligi ya Mabingwa ya CAF,” amesema Mreno huyo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuwasili.

  Kocha Jaime Pacheco amerejea Cairo kuifundisha tena klabu ya Zamalek 

  Pacheco mwenye umri wa miaka 62 alianzia kufundisha kwao, zaidi klabu ya Boavista aliyoiwezesha kutwaa taj la Ligi Kuu ya Ureno msimu wa 2000-2001. 
  Pia alizifundisha klabu za Mallorca ya Hispania, Al Shabab ya Saudi Arabia, Beijing Guoan na Tianjin Teda ya China.
  Zamalek kwa sasa inashika nafasi ya pli katika Ligi Kuu ya Misri  msimu huu, ambao tayari mahasimu wao, Al Ahly wameshajihakikisha ubingwa. Watamenyana na Raja Morocco katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF Oktoba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA MRENO PACHECO AREJEA KUINOA TENA ZAMALEK YA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top