• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 19, 2020

  BERTRAND TRAORE ATUA ASTON VILLA KWA PAUNI MILIONI 19


  Bertrand Traore akiwa ameshika jezi ya Aston Villa baada ya kukamilisha uhamsho wake kutoka Lyon kwa dau la Pauni Milioni 19 

  Matumizi ya Aston Villa tangu irejee Ligi Kuu

  2019-20

  Wesley - £22.5m

  Tyrone Mings - £20m

  Matt Targett - £14m

  Douglas Luiz - £15m

  Ezri Konsa - £12m

  Marvelous Nakamba - £10.8m

  Mbwana Samatta - £9.5m

  Trezeguet - £9m

  Anwar El Ghazi - £8m

  Tom Heaton - £8m

  Bjorn Engels - £7m

  Jota - £4m

  Kortney Hause - £3m


  2020-21

  Ollie Watkins - £33m

  Emiliano Martinez - £20m

  Bertrand Traore - £19m

  Matty Cash - £14m

  KLABU ya Aston Villa imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Burkina Faso, Bertrand Traore kutoka klabu ya Lyon ya Ufaransa kwa dau la Pauni Milioni 19.

  Mchezaj huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyeibukia katika akademi ya Chelsea na kucheza mechi 16 za kikosi cha kwanza msimu wa 2015-16, amesaini mkataba wa miaka mitatu kupiga kazi Villa Park.

  Anakuwa mchezaji wa nne mpya baada ya Ollie Watkins kutoka Brentford kwa Pauni Milion 28, zinazoweza kuongezeka hadi Milioni 33, Matty Cash kutoka Nottingham Forest kwa Pauni Milioni 14 na Emiliano Martinez kutoka Arsenal kwa Pauni Milioni 20.

  Pamoja na kusajili wachezaji wapya, Aston Villa wiki iliyopita ilompa mkataba mpya wa miaka mitano Nahodha wake, kiungo Jack Grealish ambaye sasa atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 135,000 kwa wiki.

  Hadi sasa dirisha hili, Aston Villa wametumia Pauni Milioni 84 kusajili wachezaji wapya, wakati msimu ulioptia walitumia Pauni Milioni 143 na wakaishia kunusurika kushuka daraja.

  Tangu wamerejea Ligi Kuu misimu miwili iliyopita, Aston Vlla wametumia Pauni Milioni 227 kusajili, kiwango ambacho ni Chelsea na Manchester City pekee wamekivuka kwa kipindi kama hicho. 

  Matumizi mabaya ya fedha ya Aston Villa ndani ya muda huo, yanafanana kabisa na ya Manchester United.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BERTRAND TRAORE ATUA ASTON VILLA KWA PAUNI MILIONI 19 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top