• HABARI MPYA

  Jumanne, Septemba 15, 2020

  AUBAMEYANG ASAINI MKATABA MPYA MNONO ARSENAL HADI 2023

  HATIMAYE Nahodha, Pierre-Emerick Aubameyang amesaini mkataba mpya mnono wa kuendelea na kazi Arsenal, jambo ambalo ni habari njema kwa kocha Mikel Arteta kwenye harakati zake za kurejesha makali ya timu hiyo.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amesaini mkataba mpya wa hadi mwaka 2023, ambao atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki.
  Lakini pato lake la jumla kwa wiki linaweza kuongezeka hadi Pauni 350,000 ikijumlishwa na posho, hivyo kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kikosini, akimpiku hadi Mesut Ozil.

  Nahodha, Pierre-Emerick Aubameyang amesaini mkataba mpya hadi mwaka 2023 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Gabon, Aubameyang alijiunga na Arsenal Januari 2018 kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 56 kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani na tangu wakati huo amefunga mabao 72 katika mechi 112. 

  Na tangu Arteta apewe ukocha wa Arsenal mwezi Desemba mwaka jana, Aubameyang amekuwa katika kiwango cha juu mno na kuisaidia timu kushinda Kombe la FA, hivyo kukata tiketi ya kucheza Europa League na Ngao ya Jamii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AUBAMEYANG ASAINI MKATABA MPYA MNONO ARSENAL HADI 2023 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top