• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 22, 2020

  MECHI ZA KUFUZU AFCON 2022 KUANZA NOVEMBA 9

  KAMATI ya Dharula ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imethibitisha tarehe mpya za kuanza tena kwa mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Cameroon 2022 na za makundi za kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022.
  Ratiba ngumu ya kufuzu AFCON inatarajiwa kuanza Novemba mwaka huu hadi Novemba mwakani baada ya mechi hizo kusimama tangu Machi mwaka huu kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.
  Kwa mechi za kufuzu Cameroon 2022, zitaanza Novemba 9 hadi17 mwaka huu na kuendelea baadaye Machi 22 hadi 30 mwakani.

  Timu 40 zitaanza kuwania tiketi ya Qatar 2022 kati ya Mei 31 na Juni 15 mwakani 2021 kwa kumenyana katika mechi za kwanza na za pili.
  Kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 7, mechi za tatu na za nne zitachukua nafasi, wakati mechi za tano na za sita zitafuatia Oktoba 4 had 12 mwakani.
  Na mechi za mchujo zitachezwa kati ya Novemba  8 hadi 16 mwakani kupata wawakilishi watano wa Afrika kwenye Fainali za Kombe ka Dunia 2022.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI ZA KUFUZU AFCON 2022 KUANZA NOVEMBA 9 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top