• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 22, 2020

  ARISTIDE BANCE ASTAAFU KUCHEZEA BURKINA FASO BAADA YA MIAKA 17

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burkina Faso, Aristide Bance amestaafu kuchezea timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya miaka 17.
  Bance ambaye Septemba atatimiza miaka 36, ameichezea jumla ya mechi 79 The Stallions na kuifungia mabao 24 tangu aanze kuitumika mwaka 2003.
  Bance ambaye kwa sasa anachezea vigogo wa Guinea, Horoya AC, ametoa tamko hilo jana baada ya kukutana na Rais wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kabore.
  “Nataka kutoa shukrani zangu kwake (Rais Kabore) kwa yote aliyoifanyia soka ya Burkinabe. Pia nachukua nafasi hii kumtaarifu rasmi nia yangu ya kumaliza muda wa kucheza soka ya kimataifa, mwisho wangu na Farasi Dume wa Burkina Faso na kumpa namba yangu ja bahat 15,” aemeandka Bance katka ukurasa wake wa Facebook.
  Mara ya mwisho mshambuliaji huyo kuchezea Les Etalons ilikuwa Novemba 2019 alipofunga mabao yote katika ushindi wa 2-1 dhidi Sudan Kusini kwenye mchezo wao wa pili wa Kundi B kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Cameroon 2021.
  Bance anasifika kwa kuchezea klabu nyingi duniani katika nchi za Ukraine, Ujerumani, Falme za Kiarabu, Qatar, Uturuki, Finland, Kazakhstan, Afrika Kusini, Latvia, Misri na Ivory Coast.
  Kwa sasa yupo na Horoya ya Guinea ambayo aliisaidia kufika Nusu Fanal Kombe la Shirikisho Afrika ambako walitarajiwa kukutana na vigogo wa Misri, Pyramids na amesema anaelekeza nguvu zake katika kuitumikia klabu hiyo pekee kwa sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARISTIDE BANCE ASTAAFU KUCHEZEA BURKINA FASO BAADA YA MIAKA 17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top