• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 14, 2020

  SEBASTIEN MIGNE AJIUZULU UKOCHA EQUATORIAL GUINEA

  KOCHA Mfaransa, Sebastien Migne ametangaza kujiondoa timu ya taifa ya Equatorial Guinea kwa makubaliano na uongozi. 
  Migne alijiunga na Nzalang Nacional, yaani Ngurumo ya Taifa jina la utani la timu ya taifa ya Equatorial Guinea Novemba mwaka jana na kuiongoza kwenye mechi mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Cameroon.
  “Huu ni mwisho, na janga la COVID-19 limefanya hali yangu kuwa mbaya. Familia yangu kwa sasa imekwama Kenya na sijaiona kwa miezi kadhaa. Kipaumbele changu ni wao. Kwa sasa nipo Ufaransa na hatujui lini mipaka itafunguliwa tena,” amesema Migne.

  “Ni mkanganyiko kubaki kazini bila mashindano na pia kwa Shirikisho la Soka Afrika kumlipa kocha wa kigeni bila kufanya chochote. Kitu kizuri kilikuwa ni kusitisha mkataba kwa makubaliano tuliyosaini,”aliongeza Migne.
  Baada ya kupoteza mechi mbili za kufuzu AFCON ya 2021, Ngurumo ya Taifa wamejiweka kwenye nafasi finyu ya kukata tiketi ya Cameroon mwakani, ingawa Migne bado ana matumaini.
  “Kufuzu Cameroon 2021, Equatorial Guinea lazima washinde mechi za nyumbani na ugenini dhidi ya Libya. Lazima wajaribu kupata angalau pointi nne kama si zote sita. Baada ya hapo watacheza na Tanzania nyumbani wakiwa kwenye nafasi nzuri tena"alisema Migne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SEBASTIEN MIGNE AJIUZULU UKOCHA EQUATORIAL GUINEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top