• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 22, 2020

  MESSAGER DE NGOZI YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA BURUNDI

  TIMU ya Le Messager de Ngozi imetewazwa kuwa bingwa wa Ligi Kuu ya Burundi, maarufu kama Primus Ligue ikiwa imebakiza mechi moja baada ya kuifunga Inter Star 3-0 Uwanja wa Urukundo mjini Mwumba Jumamosi.
  Ushindi huo umewafanya Le Messager wafikishe pointi 61, hivyo kuongoza ligi hiyo kwa pointi tano zaidi ya Musongati wanaoshika nafasi ya pili ambao walitoa sare ya 1-1 na Kayanza United.
  Ngozi walikuwa wamefungana na Musongati kwa kila kitu wakati ligi inarejea baada ya kusimama kwa mwezi mmoja, lakini wakashinda mechi zao tatu kati ya tano huku wapinzani wao wakishinda moja tu.

  Mabao ya juzi wakikabidhiwa taji yalifungwa na Olivier Bayizere, Iddy Museremu na Arthur Nibikora, hilo likiwa taji la pili la Ligi kwa timu hiyo ya Wilaya ya Ngozi.
  Waliokuwa mabingwa watetezi, Aigle Noir wamemaliza nafasi ya tatu kwa pointi zao 45, sawa na Dynamik na Flambeau du Centre na watatakiwa kushinda mechi yao ya mwisho kujihakikishia kumaliza ndani ya Tatu Bora.
  Wakat huo huo, Lydia Ludic, Ngozi City na Les Lierres zitateremka Daraja baada ya kumaliza mkiani mwa ligi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSAGER DE NGOZI YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA BURUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top