• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 20, 2020

  KOCHA WA MAKIPA MISRI AFARIKI KWA UGONJWA WA COVID 19

  CHAMA cha Soka Misri (EFA) kimethibitisha kifo cha kocha wa makipa Mohamed Abdo, aliyefariki dunia Mei 11 kwa ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona. 
  Abdo aliyekuwa ana umri wa miaka 59, ambaye alikuwa kocha wa makipa wa klabu ya FC Badr ya Daraja la Tatu, alipimwa na kukuta ugonjwa wa COVID-19 na alikuwa akipatiwa matibabu Kafr El-Dawar, kiais cha kilomita 180 kutoka Jiji la Cairo.
  “Familia ya soka Misri imesikitishwa na habari za kifo hicho. Tunawapa pole familia yake. Wawe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,”, imesema taarifa ya EFA.

  Shughuli za soka zimesimamshwa Misri tangu katikati ya Machi kutokana na janga hilo la maambukizi ya virusi vya corona, huku watu takriban 13,500 wameripotiwa kupatwa na virusi hivyo hadi jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA WA MAKIPA MISRI AFARIKI KWA UGONJWA WA COVID 19 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top