• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 19, 2020

  MAYANJA ASHINDA TUZO YA KOCHA BORA UGANDA FEBRUARI

  NYOTA wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, kocha Jackson Mayanja na mshambuliaji, Robert Ssentongo wameshinda tuzo za Fortebet Real Stars Sports za mwezi Februari 2020.
  Katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Cooper Chimney, Lugogo Jijini Kampala Jumatatu, Mayanja anayefundisha Kyetume FC kwa sasa aliyojiunga nayo baada ya kuachana na KMC ya Kinondoni, Dar es Salaam amewashinda Brain Ssenyondo wa Mbarara City na Abbey Kikomeko wa Busoga United.
  Kwa upande wake, Ssentongo ambaye anachezea klabu ya Kyetume FC ameshinda tuzo huyo akiwaangusha Brian Ahebwa wa Mbarara City na David Bagoole wa Busoga United.
  Kocha wa zamani wa Simba na KMC, Jackson Mayanja ameshinda tuzo ya Fortebet Real Stars Sports mwezi Februari 2020

  Chini ya Mayanja, Kyetume FC haikupoteza mechi mwezi Februari, ikishinda michezo mitatu kati ya mitano ya Ligi Kuu ya Uganda, mingine miwli ikitoa droo dhidi ya Wakiso Giants na URA. 
  Ssentongo yeye kwa mwezi huo Februari amefunga mabao sita katika mechi tano za SUPL, hivyo kuisaidia Kyetume FC kupanda hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi.
  Washindi wengine ni Kirabo Namutebi katika mchezo wa kuogelea, Joseph Cheptegei katika Riadha, Shadir Musa katika Ndondi na Aaron Ofoyroth katika Rugby. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAYANJA ASHINDA TUZO YA KOCHA BORA UGANDA FEBRUARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top