• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 19, 2020

  MAN UNITED KUMNUNUA AUBAMEYANG KWA PAUNI MILIONI 50

  KLABU ya Manchester United inajiandaa kutoa dau la Pauni Milion 50 kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang.
  Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Washika Bunduki wanaweza kumuuza mshambuliaji wao huyo nyota ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2021. 
  Viongozi wa Arsenal wamekwishakubali mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 hatasaini mkataba mpya na kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anataka kutumia fursa huyo.
  Aubameyang amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka kwenye kikosi cha Mikel Arteta baada ya timu hiyo kutolewa kwenye michuano ya Europa League na sasa inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England. 

  Manchester United iko tayari kutoa dau la Pauni Milioni 50 kumnunua Pierre-Emerick Aubameyang 

  Arsenal ilimnunua kwa dau la rekodi mwanasoka huyo wa kimataifa wa Gabon, Aubameyang kutoka Borussia Dortmund, Pauni Milioni 56 Januari mwaka 2018.
  Barcelona na Paris Saint-Germain nazo zinatajwa kuwa miongoni mwa klabu zinazowania saini ya Aubameyang na ziko tayari kutoa ofa ili akawaongezee nguvu.
  Manchester United ilimnunua Odion Ighalo kwa mkopo kutoka Shanghai Greenland Shenhua ya China January baada ya kumkosa Josh King wa Bournemouth.
  Ighalo amekuwa na mwanzo mzuri Old Trafford, lakini haijulikani atadumu kwa muda gani katika klabu hiyo ambayo inahaha kuziba mapengo ya Romelu Lukaku iliyemuuza na majeruhi Marcus Rashford na Anthony Martial msimu huu. 
  Aubameyang tayari amefunga mabao 20 kwenye mashindano yote msimu wwa 2019/2020 baada ya kufunga mabao 31 msimu uliopita.
  Mkuu wa Idara ya Soka, Raul Sanllehi na Mkurugenzi wa Ufundi, Edu walitaka Nahodha huyo wa klabu asaini mkataba mrefu.
  Lakini Sanllehi na Mkuruegnzi Mtendaji, Vinai Venkatesham pia wamesistiza wataepuka kuruda makosa waliyofanya kwa Aaron Ramsey na Jack Wilshere ambao wote waliondoka bure.
  Mesut Ozil, Bukayo Saka, Shkodran Mustafi na Reiss Nelson nao pia wanatarajiwa kumaliza mikataba yao mwaka 2021, lakini nguvu zimeelekezwa zaidi kwenye utatuzi wa suala la Aubameyang. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED KUMNUNUA AUBAMEYANG KWA PAUNI MILIONI 50 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top