• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 27, 2020

  MAGWIJI WAUNGANA KATIKA VITA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

  MAGWIJI wa soka Afrika wameungana kutoa video fupi ya kampeni dhidi ya maambukizi virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 iitwayo #MikonoSalama na #MsishikaneMikono.
  Video hiyo ya sekunde 98 imehusisha wachezaji wakiwa katika maeneo wanayoishi ikisistiza kunawa mikono na kuepuka kushikana mikono, ambayo husababisha kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19, unaotikisa dunia nzima kwa sasa.
  Wawakilishi wa vizazi tofauti wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Anthony Baffoe wameshiriki video hiyo.

  https://web.facebook.com/ConfederationofAfricanFootball/videos/2792054437529461/

  Hao ni pamoja na Roger Milla, Joseph Antoine Bell wa Cameroon, Herita Ilunga, Tresor Lomana Lualua wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), El Hadji Diouf, Alassane N’Dour, Khalilou Fadiga na Diomansy Kamara wa Senegal.
  Wengine ni Mustafa El Haddaoui wa Morocco, Jean Ssenide wa Uganda, Wael Gomaa wa Misri, Fatau Dauda wa Ghana na Vincent Enyeama wa Nigeria.
  Akina Diouf na Lualua wamezungumza kwa lugha na lafudhi za kwao, Wolof ya Senegal na Lingala ya Kongo ili kufikisha ujumbe kwa watu wa nchini mwao, wakati Mganda Ssenide ni mwanamke pekee katika kampeni hiyo.
  Kutokana na ugonjwa wa COVID-19, CAF imesimamisha mashindano yake yote hadi hapo itakapoamuliwa vingnevyo – hiyo ikiwa ni kuunga mkono agizo la Shirika la Afya Duniani (WHO), FIFA na wengine katika mapambano dhidi ya janga hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAGWIJI WAUNGANA KATIKA VITA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top