• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 03, 2020

  ABDELMOUNAIM BAH ACHUKUA NAFASI YA MOUAD HAJJI CAF

  MKURUGENZI wa Biashara, Abdelmounaim Bah ameteuliwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
  Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Kamati ya Dharula ya CAF kilichofanyika leo Jijini Cairo nchini Misri, yalipo makao makuu ya shirikisho hilo.
  Kwa ruhusa ya Rais wa CAF, Ahmad kikao cha Kamati ya Dharula kilifanyika leo na kumteua Bah kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, baada ya kukubali ombi la kujiuzulu la Mouad Hajji, aliyeng’atuka jana katika nafas hiyo.
  Wajumbe wa Kamati hiyo wana imani ya kutosha juu ya Bah ambaye amekuwa mtendaji mzuri tangu amejiunga na CAF, hususan wakati wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri mwaka 2019.
  Mmoroco huyo, Bah ameingia ofisini mara moja na kuanza kazi hadi hapo kitakapofanyika kikao kingine cha Kamati ya Utendaji ya CAF.
  Wakati huo huo, Bah ataendelea na majukumu yake ya Ukurugenzi wa Biashara, nafasi aliyopewa tangu Juni mwaka 2018.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ABDELMOUNAIM BAH ACHUKUA NAFASI YA MOUAD HAJJI CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top